Twaweza.org

JiElimishe | Uhusiano kati ya matokeo ya kujifunza na utapiamlo

Takwimu mpya zilizotolewa na Uwezo (iliyopo Twaweza) zinaonesha uhusiano kati ya matokeo ya watoto ya kujifunza na utapiamlo.

Miongoni mwa watoto wenye miaka 10 mpaka 14:

Somo la Kingereza (uwezo wa kusoma hadithi ya kingereza ya kiwango cha darasa la 2):

Watoto wenye utapiamlo – asilimia 17.9 walifaulu

Watoto wenye utapiamlo wa wastani – asilimia 16.4 walifaulu

Watoto wasio na utapiamlo – asilimia 25.8 walifaulu

Somo la Kiswahili (uwezo wa kusoma hadithi ya Kiswahili ya kiwango cha darasa la 2):

Watoto wenye utapiamlo – asilimia 46.3 walifaulu

Watoto wenye utapiamlo wa wastani – asilimia 51.3 walifaulu

Watoto wasio na utapiamlo – asilimia 65.8 walifaulu

Somo la Hisabati (uwezo wa kufanya hesabu za kuzidisha za kiwango cha darasa la 2):

Watoto wenye utapiamlo – asilimia 35.5 walifaulu

Watoto wenye utapiamlo wa wastani – asilimia 37.7 walifaulu

Watoto wasio na utapiamlo – asilimia 53.4 walifaulu

Watoto wasio na utapiamlo wanafaulu zaidi kusoma masomo ya Kiswahili na Hisabati kuliko wale wenye utapiamlo.

Matokeo haya yametolewa na Uwezo (iliyopo Twaweza) katika halfa iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Halfa hiyo ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa semina za JiElimishe zinazofanyika kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu na Twaweza. Takwimu juu ya uhusiano kati ya lishe na matokeo ya kujifunza zilikusanywa kati ya Oktoba na Desemba 2015 kutoka kwa watoto 197,451 na kaya 68,588.

Endelea kusoma: elimu

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri