Twaweza.org

Machapisho

Twaweza kupitia kituo chake cha habari,Uwazi inatoa machapisho mbalimbali kwa wananchi wa Afrika Mashariki na ulimwengu mzima ili waweze kujipatia taarifa za kuaminika na pasipo na gharama. Taarifa hizi ni mkusanyiko wa takwimu, ripoti, tafiti mbalimbaliza kisayansi na vielelezo vya sekta lengwa za Twaweza. Tutajitahidi kadiri iwezekanavyo kuzitoa katika lugha nyepesi . Tembelea kurasa hii kila wakati ujipatie mambo mapya.

< iliyopita 123...91011
77 makala
Sort by: Maoni |

Ndoa za Utotoni Hupunguza Ubora wa Maisha kwa Wasichana wadogo na Watoto wao

Nchini Tanzania, wasichana 2 kati ya 5 wameolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18. Nchi inaweza kuwa inapoteza kiasi cha Tsh milioni 637 kila mwaka (ilikadiriwa, 2015) mapato yanayopotea kwasababu ya ndoa za utotoni.

Tamko kuhusu Marekebisho yanayopendekezwa kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa

Sisi kama taasisi huru ya kiraia ambayo inalinda haki/kanuni za kidemokrasia, tungependa kutoa maoni na kupaza sauti yetu kwenye mjadala unaoendelea tukiwa na lengo la kutafuta njia bora ya kusonga mbele, ambayo italinda demokrasia yetu changa huku ikipatikana njia sahihi ya kusimamia usajili wa vyama vya siasa.

Maoni ya wananchi kuhusu ushiriki, maandamano na siasa nchini Tanzania

Uungaji mkono wa haki za vyama vya upinzani nao pia umeongezeka. Asilimia 37 ya wananchi wanasema vyama vya upinzani vinapaswa kuikosoa na kuifuatilia serikali ili kuiwajibisha mara baada ya vipindi vya chaguzi kuisha ukilinganisha na asilimia 20 tu walisema hivyo mwaka 2016.

Elimu bora au bora elimu? Elimu waitakayo watanzania

Utafiti huu umebaini kwamba ni wazazi wachache sana huzingatia ada nafuu (6%) na umbali wa shule (18%) wakati wa kuchagua shule za sekondari kwa ajili ya watoto wao. Badala yake wazazi wengi huzingatia zaidi viwango vya juu vya ufaulu wa shule husika (asilimia 72) na walimu wanaojituma (asilimia 72 pia).

Siyo kwa kiasi hicho? Maoni ya watanzania kuhusu taarifa na mijadala

Wananchi wengi wana imani kubwa na taarifa zinazotolewa na Rais (70%) na Waziri Mkuu (64%). Idadi ndogo zaidi wanamwamini mwenyekiti wao wa kijiji (30%), wabunge (wa chama tawala 26%, wa upinzani 12%), na viongozi wa serikali kwa ujumla (22%).

Afya Kwanza: Wasemavyo wananchi kuhusu huduma za afya

Wananchi wanapopata majeraha ama kuugua, 6 kati ya 10 (61%) huenda katika kituo cha afya cha serikali. Kiwango hiki kimeongezeka kutoka 45% mwaka 2014 na kubaki hivyo hivyo tangu mwaka 2016.

Hapa Usalama Tu | Usalama, haki na polisi nchini Tanzania

Kuna mtazamo wa jumla miongoni mwa wananchi kuwa usalama nchini umeimarika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kama inavyooneshwa na zaidi ya nusu ya wananchi hao (asilimia 53).
< iliyopita 123...91011
77 makala
Sort by: Maoni |

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri