Twaweza.org

Hali Halisi: Maoni ya wananchi juu ya elimu bila malipo ya ada.

Kufuatia kuanzishwa kwa mfumo wa elimu bila malipo ya ada, asilimia 50 ya wananchi wanasema ubora wa elimu umeongezeka. Lakini asilimia 35 wanasema ubora wa elimu umebaki palepale huku asilimia 15 wakisema umeshuka.    

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wake Hali halisi: Maoni ya wananchi juu ya elimu bila malipo ya ada. Muhtasari huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa na unaotumia simu za mikononi. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,806 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara kati ya tarehe 7 na tarehe 14 agosti 2016. (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya)                    

Wananchi wengi wana mitazamo chanya juu ya elimu nchini Tanzania, lakini, ni dhahiri kuwa shule za serikali bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kwa mujibu wa wahojiwa, changamoto kuu ni ukosefu wa walimu (imetajwa na asilimia 34), madawati (asilimia 30) na madarasa (asilimia 13), pamoja na uhaba wa vitabu (asilimia 7).

                         

                         

   

Endelea kusoma:

Editors: Aidan Eyakuze

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri