Twaweza.org

Je, juhudi za serikali zimesaidia vita dhidi ya rushwa? Mtazamo wa watu kuhusu rushwa nchini Tanzania

Wananchi wanaiona rushwa katika sekta zote za huduma za Serikali kama kitu cha kawaida kabisa. Sekta zinazoongoza kwa rushwa ni pamoja na polisi (94%), siasa (91%), afya (82%), kodi (80%) , ardhi (79%), elimu (70%), serikali za mitaa (68%) na maji (56%). Pia wananchi 50% wanaona mashirika yasiyo ya kiserikali nayo yanajihusisha na rushwa. Sekta pekee zinazoonekana kuwa na viwango vya rushwa chini ya 50% ni zile za biashara pamoja na mashirika ya dini.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wenye jina la Je, juhudi za serikali zimesaidia vita dhidi ya rushwa? Mtazamo wa watu kuhusu rushwa nchini Tanzania. Muhtasari umetokana na utafiti wa Sauti za Wananchi; utafiti wa kwanza Afrika kwa njia ya simu mkononi wenye uwakilishi wa kitaifa, ambao ulikusanya maoni kutoka Tanzania Bara.

Mbali na mitazamo kuhusu rushwa, Twaweza iliuliza kuwa ni wakati gani hasa wananchi huombwa rushwa? Kwa mara nyingine, polisi waliongoza katika hili: wananchi watatu kati ya watano (60%) waliombwa rushwa mara ya mwisho walipokutana na polisi. Wananchi wawili kati ya watano (41%) walilipa rushwa hiyo, na wananchi 2% walitoa rushwa wenyewe bila kuombwa. Aina ya pili ya rushwa iliyoonekana kutendeka kwa kiasi kikubwa ni wakati wananchi wanatafuta kazi: mtu mmoja kati ya watatu (34%) aliombwa malipo yasiyo rasmi alipokuwa akitafuta kazi.

Endelea kusoma:

Authors: Angela Ambroz

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri