Sauti za Wananchi

To read this in English, go here.
Uwazi iliyopo Twaweza imezindua utafiti wa awali wa Sauti za Wananchi (Voices of Citizens), ambao ni mradi mpya unaotumia simu za mkononi ili kukusanya taarifa za mara kwa mara kutoka katika wigo mpana wa wananchi wa Tanzania. Mradi huu utawezesha data za awali/msingi kukusanywa kwa haraka na kwa ufanisi, kwa gharama ya chini, kuwataarifu wananchi kuhusu yale yanayoendelea na kuwasaidia watunga sera kushughulikia kwa ukaribu zaidi mahitaji na matamanio ya raia. Zaidi
Tafiti , ni njia ambazo watunga sera na wahisani hutumia kukusanya taarifa kuhusu ufanisi wa utendaji wao na pia vipaumbele vya wananchi, mara nyingi huwa zina gharama kubwa na zinazochukua muda mwingi. Mara nyingine huchukua hadi miaka miwili tokea wazo liibuliwe hadi data zinapopatikana. Mradi wa Sauti za Wananchi unakusudiwa kupunguza pengo hili ili kwamba pande zote zinazohusika ziweze kupata data kwa urahisi, mara kwa mara na zinazohuishwa mara kwa mara kuhusu hali halisi ya maisha ya wananchi.
Wakati ambapo idadi ya tafiti hizi mara nyingi huwa zina ukomo wa wigo na upana wa maeneo ya kufikia – kuanzia kwa washiriki na hata eneo la kijiografia la ushiriki – Mradi wa Sauti za Wananchi unalenga kutoa data za kila mwezi kuhusu mada mbalimbali kwa mapana na marefu yake kwa sampuli ya uwakilishi wa washiriki 2,000 kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Mradi utakuwa na awamu mbili: katika awamu ya kwanza, Utafiti wa awali n a mahojiano katika kaya, washiriki 2,000 wataombwa kuwa watoa taarifa wa Sauti za Wananchi na watakabidhiwa simu ya mkononi pamoja na kifaa cha kuchajia simu kinachotumia nishati ya jua. Katika awamu ya pili, washiriki watakuwa wakipigiwa simu kila mwezi kutoka katika kituo cha mawasiliano ambapo wataulizwa maswali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maisha yao. Baada ya miezi kadhaa matayarisho a, hatimaye utafiti wa awali ulizinduliwa jijini Dar es Salaam mwezi Oktoba 2012. Utafiti wa awali awamu ya kwanza unatarajiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka 2012.
Twaweza ina matumaini kwamba utaratibu umakini na mbinu ya kufanyika mara nyingi ya Sauti za Wananchi utatoa njia mpya yenye msukumo mkubwa kwa wananchi kuiubua aina ya jamii wanayotaka na kufanya maamuzi ya kisera nchini Tanzania na katika nchi nyinginezo. Licha ya ripoti za kila mwezi, Twaweza inakusudia kuwezesha upatikanaji wa data kamili kupitia mtandao wa intaneti ili watafiti wazitumie kufanya uchambuzi wao.
Tanzania: Ushiriki, maandamano na siasa
5 Jul 2018
|
Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua
Wanapotathmini viashiria mbalimbali vya demokrasia, wananchi wengi wanasema uhuru umepungua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Wananchi wanasema uhuru umepungua kwa vyama vya upinzani kufanya mikutano na kutoa maoni yao (64%), vyombo vya habari kukosoa au kuripoti maovu ya serikali (62%), na makundi yasiyofungamana na upande wowote kupaza sauti zao na kufanya mikutano (58%). Nusu ya wananchi pia wanaona hawana uhuru wa kuonesha mitazamo yao ya kisiasa (54%).
Tanzania: Elimu bora au bora elimu?
16 May 2018
|
Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua
Muhtasari huu unawasilisha maoni ya wananchi kwenye na masuala yanayohusiana na sera ya elimu. Utafiti huu umebaini kwamba ni wazazi wachache sana huzingatia ada nafuu (6%) na umbali wa shule (18%) wakati wa kuchagua shule za sekondari kwa ajili ya watoto wao. Badala yake wazazi wengi huzingatia zaidi viwango vya juu vya ufaulu wa shule husika (asilimia 72)
Tanzania: Siyo kwa kiasi hicho?
28 Mar 2018
|
Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua
Muhtasari huu umebeba takwimu zinazohusu mitazamo na uzoefu wa wananchi kuhusu upatikanaji wa habari na mijadala. Unaripoti kuwa wananchi 7 kati ya 10 wanasema taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma ni mali ya umma (70%, juu zaidi kutoka 60% mwaka 2015); na wananchi 9 kati ya 10 wanasema wananchi wa kawaida wapate taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma (86%, juu zaidi kutoka 77% mwaka 2015) na kwamba kwa kuwapa wananchi uwezo wa kupata taarifa kunaweza kupunguza rushwa (86%, juu zaidi kutoka 80% mwaka 2015).