Twaweza.org

Tathmini

Mojawapo ya  vipaumbele vya Twaweza ni kujifunza kupitia tafakuri juu ya matendo yetu na kuchangia kupeana mafunzo. Jambo la msingi katika haya ni tahmini ya kazi za Twaweza. Na tutatumia tathimini huru kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa miaka mitano ya kwanza ya uhai wa Twaweza. Wakati jambo hili ni huru,yaani tathimini ya nje,ukweli ni kwamba itajumuishwa na ufatiliaji wetu pamoja na mifumo na michakato ya utathimini ya ndani. Tutazingatia majibu yatokanayo na masomo toka kwa watathimini huru kama michango kwa kujifunzia na tafakuri zetu,na kuiiunga nao ili kuleta usimamizi wenye kukubali mabadiliko na mipango.

Utangulizi wa kazi ya tathimini umekwishafanywa na Kituo cha Elimu ya Kimataifa (CIE) cha Chuo Kikuu cha Massachussetts huko Amherst.Muundo  wa tathmini hiyo utajumuisha njia mbali mbali za utafiti (za kimahesabu na ki-maelezo) utakaokuwa na madhumuni ya kuchunguza matokeo mapana katika medani za utashi wa raia na upatikanaji wa huduma, kupitia utafiti wa msingi na uchunguzi wa mwendelezo. Ili kufuatilia matokeo haya pamoja na dhana ya hali-muundo chunguzi nyingine ndogo zaidi zimepangwa. Hizi ni pamoja na chunguzi mahsusi zitakazoendelea kwa muda wote wa miaka mitano, na zinaweza pia kujumuisha chunguzi za kijamii kwa kutumia njia fupi za kimajaribio. Utafiti wa msingi, ambao utajumuisha tafiti za kaya, jumuiya pamoja na utafiti kuhusu huduma utakamilika ndani ya mwaka 2010. 

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri