Twaweza.org

Ufuatiliaji

Uwajibikaji kwa kazi zetu ni jambo muhimu sana kwetu. Badala ya kuona uwajibikaji kama sharti lililolazimishwa kutoka nje, tunauona kama sehemu muhimu ya kuimarisha ufanisi wa miradi yetu na kujifunza, na pia kama njia ya kuwapatia watathamini kutoka nje taarifa muhimu. Katika mwaka 2010 mifumo itawekwa kwa ajili hii. Ufuatiliaji unaowahusu wabia au washirika hauna budi kuchangia katika uimarishaji wa ufuatiliaji wa ubia wa kimkakati na hatimaye uweze kuimarisha ufuatiliaji wa Twaweza kwa ujumla. Twaweza yenyewe imekwisha kubuni mfumo wa mipango na bajeti za mwaka ambazo zinaunganishwa na maelezo pamoja na taarifa za mahesabu yaliyokaguliwa zilizojikita katika matokeo na vigezo vya msingi. Asasi za wabia wetu zitasaidiwa kutengeneza mifumo kama hii kila itakapohitajika. Katika ngazi ya ubia, ufuatiliaji utajengeka juu ya misingi iliyojengwa na asasi husika, lakini pia utanufaika kutokana na utaratibu wa utafiti na matumizi ya fomu za mrejesho na mazoezi ya mafunzo na tafakuri. Ufuatiliaji wa Twaweza kwa ujumla utanufaika na mifumo hii kwa ujumla na utakuwa ni sehemu ya tathmini huru kutoka nje.

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri