Twaweza.org

Wabia

Kiini cha mtazamo wa Twaweza ni ubia katika kutekeleza programu zetu. Kupitia ubia wa kimkakati na wa aina mpya, Twaweza inakusudia kuchangamsha uundaji wa miundo-hali inayowawezesha wananchi kukuza utashi wao na wakaweza kupata taarifa, kusimamia maendeleo, kupaza sauti zao na kuleta mabadiliko na kwa kufanya hivyo, kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa umma. Tunashirikiana na wabia wanaojihusisha na sekta za maji, afya na elimu, lakini pia tunashirikiana na wabia wanaounga mkono ukuzaji wa utashi wa raia kwa ujumla. Mojawapo ya vigezo muhimu tunayoyaangalia katika kujenga ubia ni upana wa mtazamo na uwezo wa kuwafikia watu wengi. Kanuni mojawapo ni kushirikiana na wabia wenye mashiko ya kitaifa na wanaowanufaisha angalau watu wapatao milioni mbili, pamoja na walio maeneo ya vijijini.Kwa habari zaidi kuhusu vigezo na masharti yetu kuhusu ubia, soma zaidi.

Tunapenda kukutaarifu kuwa mikondo mipya ya ubia inaandaliwa tangu mwanzoni mwa mwaka 2010. Angalia katika sehemu hii kwa ajili ya taarifa zaidi katika miezi ijayo.

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri