Twaweza.org

Kujifunza

Pamoja na kwamba Twaweza imejikita sana katika utendaji, lakini pia inathamini sana kujifunza. Tukiziweka nguzo hizi kuu katika nadharia yetu ya mabadiliko  katika maswali, tunaweza kupata maswali yafuatayo:

  • Ni jinsi gani upatikanaji wa taarifa- ikijumuisha nyenzo na mikondo ya upatikanaji taarifa au habari unaweza kupanuliwa kwa mapana katika nchi za Afrika Mashariki?
  • Je, uboreshaji wa upatikanaji wa habari utaimarisha utashi wa raia (uwezo wa raia kuwa na udhibiti mkubwa zaidi juu ya maisha yao na kuleta mabadiliko?
  • Je, uboreshaji wa upatikanaji wa habari na uimarishaji wa utashi wa raia vinachangia kwa kiwango kikubwa katika uboreshaji wa huduma muhimu (katika afya, elimu na maji) na kuwawezesha wananchi kuleta mabadiliko katika maeneo mengine yanayowagusa?
  • Ni mchango gani Twaweza imetoa kwa mabadiliko haya?

Tunapenda kuweza kuyajibu maswali haya. Ingawaje juhudi zetu zimejengeka juu ya uzoefu uliopatikana kwingineko duniani, lakini tunajaribu mbinu mpya zisizo za kawaida wakati tukijenga ubia na asasi nyingine. Tunahitaji ushahidi madhubuti kuhusu jinsi ambavyo utashi wa raia unavyoweza kuleta mabadiliko endelevu katika maisha ya wananchi. Tumekusudia kuisaili dhana yetu ya utashi wa raia na kuutafsiri ushahidi huo katika mafunzo tunayoweza kubadilishana ndani ya Twaweza yenyewe, miongoni mwa wabia wetu na katika jamii iliyo pana. Ndiyo maana kujifunza na mawasiliano vimepewa kipaumbele cha hali ya juu na pia kwanini ubunifu, kujifunza, ufuatiliaji na uwasilishaji wa mafunzo ni mihimili muhimu ya mtazamo wa Twaweza.

Twaweza inawahimiza wabia wake kutafakari utendaji wao na kujenga utamaduni wa kujifunza, pamoja na kujikosoa kwa kujua kwamba kutofanikiwa ni nafasi nyingine ya kujifunza na kubuni mbinu mbadala. Tunasisistiza juu ya mafunzo na malezi ya muda mrefu na kuwapeleka wanafunzi wa vyuo vikuu wa Afrika Mashariki na kwingineko miongoni mwa wabia wetu, mahsusi kwa ajili ya kukusanya, kuhifadhi na kuwasilisha nyaraka. Aidha tunashirikiana kwa karibu na watathamini wetu (huru) wa nje ili kupata mrejesho kutokana na utafiti wao katika kazi zetu.

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri