Twaweza.org

Vyombo vya habari

Twaweza inakupatia mchanganyiko wa taarifa tofauti kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Hivi vinajumuisha vyombo vipya kama tovuti, radio,televisheni,machapisho au majarida pamoja na magazeti pia.

< iliyopita 123...8910
68 makala
Sort by: Maoni |

Uwezo yaunga mkono mabadiliko katika mfumo wa elimu nchini Kenya

Mratibu wa Uwezo nchini Kenya, Dr. John Mugo anaunga mkono mabadiliko yaliyopendekezwa tume iliyoteuliwa na Serikali kwenye mfumo wa elimu nchini Kenya, limeripoti gazeti la Daily Nation. Tume hiyo ya wajumbe 35 imeshauri kuwa Serikali iondokane na mfumo wa 8-8-4 (miaka minane ya elimu ya msingi, minne ya sekondari na minne ya chuo kikuu), ulitekelezwa tangu 1985,na badala yake kuweka mfumo wa 2-6-6-3 ( miaka miwili ya elimu ya awali, sita ya elimu ya msingi, sita ya elimu ya sekondari mitatu ya chuo kikuu)

Mugo anasema mfumo unaopendekezwa utakuwa bora kwa wanafunzi, kwa kuwa msisitizo utakuwa si kufaulu madarasa bali ni kupata stadi zinazotakiwa. Pia wanafunzi watapata mapema mwelekeo wa kazi gani wangependa kufanya baadaye maishani. Mugo alikuwa akiongea katika uzinduzi wa ripoti ya mwaka ya ujifunzaji mapema wiki hii. Soma zaidi.

Changieni mawazo mjadala wa elimu, Uwezo Kenya yasema

Mratibu wa Uwezo Kenya, Dr. John Mugo anawapa moyo Wakenya kusoma ripoti ya hivi karibuni kuhusu mapendekezo ya mabadiliko kwenye mfumo wa elimu wa Kenya na kutoa mawazo yao. Ameliambia The Star kuwa wadau wa elimu wanapaswa kutumia nafasi ya mkutano wa mashauriano kutoa mawazo yao kuhusu sera ya elimu ya nchi hiyo. Soma zaidi.

Walimu wakuu waadibishwa kwa matokeo mabaya ya mitihani

Katika wilaya moja nchini Uganda, walimu wakuu wameadibishwa na mamlaka za elimu kwa ufaulu mdogo wa wanafunzi katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011. New Vision linaripoti kuwa kati ya shule 121 zinazoendeshwa na Serikali katika wilaya ya Hoima ni 23 tu ndio zina angalau mwanafunzi mmoja aliyepata alama za daraja la kwanza. Maafisa Elimu wa wilaya ya Hoima wanasema watatuma barua ya onyo kwa walimu wakuu wote wa shule ambazo hazina wanafunzi waliopata daraja la kwanza. Iwapo hakutatakuwa na mabadiliko katika mitihani ijayo walimu wakuuu wanaweza kufukuzwa kazi.

Walimu wakuu katika wilaya hiyo wanasema pamoja na juhuzi zao kubwa, kuna mazingira ambayo ni juu ya uwezo wao. Wanakabiliana na upungufu wa waalimu na mishahara midogo kwa walimu waliopoa, madarasa yaliyofurika wanafunzi, uhaba wa miundombinu na vifaa.

Utafiti wa upimaji wa kujifunza wa Uwezo 2011 ulibaini ujifunzaji haba katika kusoma na kuandika kati ya watoto wa umri wa shule ya msingi nchini Uganda. Soma zaidi.

Changamoto za elimu nchini Uganda hazijapata majibu

Mnamo mwaka 2007 Serikali ya Uganda iliwekeza sana katika sekta ya elimu: zaidi ya madarasa 4,000 yalijengwa, uwiano wa walimu na wanafunzi uliboreshwa na usafi uliboreshwa mashuleni. Miaka mitano baadaye, nchi bado inasubiri kuona matokeo ya uwekezaji huo katika uwezo wa watoto kimasomo. Matokeo yaliyotoka hivi karibuni ya Mtihani wa Elimu ya Sekondari 2011 yanaonesha kupanda kidogo kwa ubora wa ukilinganishwa na miaka iliyopita. Tangu 2008 hadi 2010 asilimia ya wanafunzi wanaopata alama za daraja la kwanza imekua inapungua.

Meneja Utafiti wa Uwezo Uganda, Grace Maiso, imeliambia Daily Monitor kuwa uwiano wa walimu na wanafunzi bado si mzuri na walimu wanalipwa kidogo sana, hivyo kusababisha ufaulu mdogo wa wanafunzi. Soma zaidi.

Wahitimu darasa la 7 hawajui kusoma

Wabunge watano wang'ara

Wanafunzi wengi hawajui kusoma, kuandika-Utafiti

< iliyopita 123...8910
68 makala
Sort by: Maoni |

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri